- betty k
- Betty 1
- 001
- betty.2
- 002

Mwanahabari Betty Kyallo amempa bonge la jibu jamaa mmoja aliyedai kwamba ana uhusiano wa kipamenzi na gavana 001, Ali Hassan Joho wa Mombasa.

Alasiri siku ya Alhamisi jina la Betty lilitamba katika mitandao ya kijamii baada ya kibeti cha rangi ya hudhurungi  kinachofanana na chake kuonekana chini ya meza katika picha ya mbunge wa Suna East Junet Mohamed na gavana wa Mombasa Hassan Joho wakiwa ndani ya ndege ya kibinafsi.

Junet na Joho walisafiri nchini Dubai katika ndege ya kibinafsi kumtembelea kinara wa Nasa Raila Odinga ambaye amekuwa mjini humo kwa majuma kadhaa akipokea matibabu.

Soma pia;

Wengi walidai kuwa Betty alikuwa katika ndege hiyo na kuzamia mitandao ya kijamii kueneza uvumi dhidi yake. Kwa upande wake mwanahabari huyo ambaye alitalikiana na mumuwe Dennis Okari, alijibu kupitia kwa video aliotuma kwa mitandao ya kijamii  akivinjari mitaa kadhaa ya Nairobi katika gari lake.

Kwa kinaya alionekana akicheka uvumi kwamba alikuwa mwenye kibeti hicho na alikuwa Dubai akisema kwamba hakuwa Dubai bali alikuwa mjini Nairobi akitafuta mahali pa kula nyama choma.

Soma pia;

Mmoja wa mashabiki wake kwa jina Wajudah alimkashifu kwa kuwa katika uhusiano na gavana 001, aliandika;

KUBE UNAPEAGA JOHO! 😁😁😁BIBI YAKE ATAKUCHOMA

Betty naye bila kusita akajibu kwa kombora lenye uzito sawa,

@WAJUDAH012 TULIKUWA PAMOJA?.

Haya hapa ni majibu ya baadhi ya wafuasi wake kuhusu uvumi huu.

raidarmax Madam kwani you drove back from Dubai? I saw you on Obare Airways 🤣🤣

mike.sonko 😂😂

caren_wasike We thank God you arrived safely 😍😍😍

ngugi_ig Keep shining gal. If they can’t stay without talking about you, then you got something they desire to have but have not.

View Comments