eqrk9kpTURBXy9jNDM2MzQ1MTA2ZGUwYjgxNDgyNzc5NjI2MDk3ZTBlNi5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB

Wakuu wa polisi katika kituo cha polisi cha Athiriver ni miongoni mwa watu,15, walio hojiwa na makachero wa DCI kuhusiana na mauaji wa watoto wawili Athiriver.

Watoto hao Henry Jacktone,4, na Alivina Mutheu,3, walipatikana wakiwa wamekufa katika gari moja lililokuwa limeegeshwa katika kituo cha polisi cha Athiriver mnamo,Julai,1, mwaka huu.

Wengine waliohojiwa na makachero hao ni wafanyakazi watatu wa tingatinga lililosongesha gari hilo, hii ni baada ya madai ya mwenye gari kuwa alipata gari lake limrsongeshwa na mahala alipoliacha awali baada ya kufanya ajali.

Wachunguzi kwa sasa wanaamini kuwa watoto hao walizirai walipokuwa kwenye gari hilo na wala hawa kuuwawa kama vile ilivyosemekana awali.

Upasuaji wa mwili uliofanywa mapema wiki hii hukuonyesha kuwa watoto hao walikuwa na majeraha yeyote kwenye mwili wao,huku wengi wakiachwa na maswali mengi bila majibu.

Daktari wa watoto aliyefanya upasuaji huo Johansen Odour, alisema kuwa inaweza kuwa watoto hao walikanyagwa na gari na kisha mwenye kutekeleza kitendo hicho kukimbia.

Wazazi wa watoto hao walisema kuwa wanawe hawawezi kuwa wamezirai walipokuwa kwenye gari hilo kwa maana umbali wa kutoka  nyumbani hadi kwenye kituo cha polisi ni mrefu.

Je nani alitekeleza kitendo hicho na kuchukuwa maisha ya watoto hao wasio na hatia? ni maswali ambayo hayana majibu akilini mwa wazazi wa watoto hao na watu wengi.

View Comments