AAGk9kpTURBXy9lNmMwYzhhOThlYTVkZjk4NzM4MGVjMzY4ZGY3OTkxNy5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB

Hata baada ya rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la makanisa,mahekalu na misikiti kufunguliwa mapema wiki hii, Msikiti wa Jamia na makanisa,4, maarufu wamekaidi amri hiyo na kusema kuwa hawatafungua.

Hii ni baada ya maenea hayo ya kuabudu kufungungwa Machi mwaka huu kwa ajili ya janaga la corona.

Wahubiri wa maeneo hayo walisema kuwa watu  au washiriki 100, hawatoshi kwenye misikiti na makanisa hayo.

"This is because the guidelines issued to limit prayers to only 100 persons per session are not practical for Jamia Mosque Nairobi given its centrality in the Central Business District of the capital city." Ujumbe wa Msikiti wa Jamia Ulisoma.

Msikiti wa Jamia una washiriki, 5000, na wanapofuata agizo la kutotangamana na watu kwa mita moja washiriki watakaohudhuria ni 1700.

Pia maeneo hayo yana wafanyakazi 120, huku agizo la rais washiriki mia moja wanapaswa kuhudhuria ibada watakuwa tu wafanya kazi peke yao.

Makanisa hayo,4, ambayo yamesema kuwa hayatafungua ni kama vile yafuatayo, All Saints Cathedral, CITAM assemblies, Jubilee Christian Church na Parklands Baptist Church.

Askofu Ambrose Nyangao wa kanisa la PBC alisema kuwa kanisa hilo lina washiriki elfu mbili, ambapo wengi wa washiriki katika kanisa hilo ni familia.

Askofu David Oginde (CITAM) na Allan Kiuna (JCC) walisema kuwa ibada zao zitaendelea kuwa kwenye mitandao ya kijamii kama awali.

View Comments