Kenya siku ya jumatano imesajili visa 461 vya corona  na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa 11,252 hadi kufikia sas .

Visa hivyo ni kutoka sampuli 4,261 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita .

Wagonjwa wengine 51 wameruhusiwa kwenda nyumbani  na kufikisha jumla ya watu 3,068 ambao wamepona ugonjwa huo .

Katibu wa utawala wa wizara ya afya  Rashid Aman  amewashukuru wahudumu wa afya kwa juhudi zao kukabiliana na ugonjwa huo .watu wenginesaba wameaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha 209 walioaga dunia hadi sasa kutokana na virusi vya Covid 19

View Comments