Safari za ndege ndani ya nchi zaanza rasmi
Kenya imerejelea safari za ndege ndani ya nchi huku ndege ya kwanza ya KQ ikianza safari kutoka Nairobi kwenda Mombasa Jumatano asubuhi.
Ndege hiyo ya Kenya Airways iliondoka uwanja wa JKIA saa nne na robo asubuhi baada ya waziri wa uchukuzi James Macharia kuongoza hafla ya kuanzisha safari hiyo.
Ndege nyingine ndogo ya KQ ilitoka Nairobi kwenda Kisumu
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari hizo, Macharia amesema Kenya sasa inatarajia kuanza safari za kimataifa.
Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kwamba safari za ndege ndani ya nchi zitaanza Julai tarehe 15 ilhali zile za kimataifa zitaanza Agosti Mosi. Safari hizo zitaendeshwa kwa kufuata masharti yote na mwongozo wa wizara ya afya na mamlaka ya kusimamia safari za angani.
Uhuru aliongeza kwamba mahitaji zaidi ya kudumisha usalama wa kiafya wa wasafiri na wahudumu yatatekelezwa katika maeneo ya kuanzia safari na zinakotua ndege. Mwezi Machi serikali ilifutilia mbali safari zote za ndege za ndani na nje ya nchi