Bintiye Mandela Zindzi alipatikana na virusi vya COVID 19
Zindzi Mandela, bintiye rais wa zamani wa afrika Kusini Nelson Mandela alipatikana na virusi vya corona katika siku ambayo aliaga dunia .
Aliaga dunia katika hospitali moja jijini Johannesburg mapema wiki hii akiwa na umri wa miaka 59 .
Mwanae Zondwa Mandela ameliambia shirika habari la SABC kwamba haijabainika iwapo ugonjwa huo ndio uliosababisha kifo chake . Familia hiyo inangoja ripoi ya upasuaji wa mwili wake
" kwa sababu kulikuwa na kiimo kilichoonyesha kwamba alikuwa na COVID 19 inabidi tufuate kanuni zilizopo sasa kuhusu jinsi ya kuwazika watu wenye virusi hivyo’ amesema
Amenukuliwa akisema mamake atazikwa ijumaa asubuhi
Zindzi alikuwa balozi wa Afrika kusini nchini Denmark .
Alizaliwa Disemba tarehe 23 mwaka wa 1960 kwa Nelson Mandela na Winnie Mandela .
Zindzi amewaacha watoto wanne , Zoleka, Zondwa, Bambatha na Zwelabo.