wauguru

Mbunge  wa  Moiben Silas Tiren amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa kamati ya bunge kuhusu kilimo ili kuichukua afasi ya  mbunge wa mandera kusini Adan Ali .

Ali  alikuwa miongoni mwa washirika 16 wa  naibu wa rais William Ruto kupigwa shoka kutoka kamati za bunge  mwezi jana na mageuzi yaliyoendeshwa na rais Uhuru Kenyatta . Mbunge huyo wa Moiben  alichaguliwa bila kupingwa siku ya alhamisi .

Mwakilishi wa akina mama wa  Laikipia  Catherine Waruguru alichaguliwa kuwa  naibu mwenyekiti wa kamati hiyo .anaichukua nafasi ya  mbunge wa Navakholo Emmanuel Wangwe,  aliyeteuliwa kuwa kiranja .Tiren  anaichukua nafasi hiyo alioyolazimika kuiacha baada ya Chama cha Jubilee kumpendelea Ali mwaka wa 2018.

Mbunge wa Shinyalu  Justus Kizito  na mwakilishi wa akina mama wa Nyamira  Jerusha Momanyi  walichaguliwa kuwa mwenyekiti na naibu mwenyekiti wa kamati ya matangazo na  makataba .walichaguliwa bila kupingwa .mbunge wa Limuru Peter Mwathi na mwenzake wa chepalungu  Gideon Koske  watahudumu katika kamati ya bunge kuhusu leba na huduma za kijamii kama mwenyekiti na naibu wake mtawalia .

Upande wa walio wengi na wachache tayari zimekubaliana kuhusu uongozi wa kamati mbali mbali  na uchaguzi utakuwa tu kama njia rasmi ya kuidhinisha mwafaka huo . Kwa mfano mwakilishi wa akina mama wa Homabay Gladys Wanga  amependekezwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango  na naibu wake atakuwa mbunge wa Roysambu  Waihenya Ndirangu

 

View Comments