Kinoti apata pigo baada ya mahakama kusema ni Haji pekee mwenye uwezo wa kufungulia mashtaka
Mkurugenzi wa idara ya mahakama hana maamlaka ya kufungulia yeyote mashtaka ila kwa idhini ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Noordin Haji ,mahakama imeamuru.
Hii ni baada ya kuzuka malumbano kati ya afisi hizo mbili kuhusu aliye na maamlaka zaidi kuhusiana na kuwafunguliwa washukiwa mashtaka .
Jaji George Odunga alhamisi ameamuru kwamba DPP ndiye mwenye maamlaka ya kufungua na kumshtaki mtu. Hatua hiyo ilijiri baada ya mkuu wa maamlaka ya ukusanyaji wa raslimali za maji Geoffrey Sang kwenda kortini akipinga kukamatwa na DCI . Sang alikamatwa mwezi Aprili kwa kushukiwa kuhusika na sakata ya uporaji wa fedha za kujengwa mabwawa .
" DCI hana maamlaka wala uwezo wa kuanzisha mashtaka dhidi ya mtu yeyote ila kwa idhini kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma’ jaji Odunga amesema.
Odunga aliikosoa idara ya DCI kwa kumkamata Sang bila waranti .