Bwana Onyango 39, alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Akoth 34, waliokosana mwaka wa 2016 baada ya bwana huyo kwenda nje ya ndo.Hata baada ya kuomba msamaha, mkewe hakuweza kukaa kwa ndoa.

Wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili baada ya kuwa katika ndoa hiyo kwa karibu miaka 11.

"Msichana ambaye nilikuwa na mpango wa kando naye nilikuwa nataka kumuoa kama mke wa pili, baada ya hapo mke wangu alikuja Kakamega mtaani nilipokuwa naishi na mpango wa kando

Aliniambia niende nyumbani tukazungumze, nlipoenda alikataa maneno yangu, niliachana na mpango wangu wa kando wakati niliona maneno hayo yameleta mambo mengi

Kijana wangu mwaka wa 2018 aliniambia kuwa ana mwanamume mwingine, lakini huyo alikuwa mpango wa kando wake kwa hivyo kwa sasa hana mtu." Alieleza Onyango.

Baada ya mke wake kupigiwa simu, hakupkea simu naye Onyango alikuwa na haya ya kueleza,

"Nikiuliza mke wangu ni nini mbaya  ananiambia niende nikamuone baba yake, nikienda kwa baba yake ananiambia niende nikamuone mjini Nairobi

Na tena wanataka nipeleke mahari yaani wananipeleka kama punching bag."

Unaweza kumpa Onyango ushauri upi, aoe mke mwingine au aweze kung'ang'ana apate mkewe wa kwanza?

View Comments