mGILU kALONZO

Siasa za Ukambani zinakaribia kugeuka kipute kikali cha ubabbe kati ya gavana wa Kitui Charity Ngilu na kiongozi wa Wiper Kalonzo  Musyoka uchaguzi wa 2022 unapokaribia .

Kuna kambi mbili  ambazo zinataka kuwa na ushawish na kuamua mwelekeo wa jamii hiyo kisiasa na kumpiga konde  Kalonzo anayechukuliwa kama kiongozi wa jamii hiyo kisiasa .Kambi hizo ni  moja inayoongozwa na magavana   Charity Ngilu, Kivutha Kibwana wa makueni na Alfred Mutua wa  Machakos. Kambi nyingine inaongoza na aliyekeuwa  seneta wa Machakos Johnstone Muthama ambao inamwunga mkono naibu wa rais William Ruto .

Muthama,  kwa upande wake ameliambia gazeti la The Star kwamba  Kalonzo na Ngilu wamekuwa na tofauti za tangu jadi .Seneta huyo wa zamani wa Machakos amechekelea kwa bezo mwafaka wa ushirikiano kati ya  Kalonzo na Uhuru akisema hautabadilisha chochote .

“ Anafikiria  [Kalonzo] Uhuru  atamuachia kiti hicho. Hakuna uongozi wa kurithi Kenya  ,wakenya wataamua mkondo wanaotaka wenyewe’ Muthama amesema

Ameongeza  kwama Ngilu hunda anatuia njama yake dhidi ya kalonzo ili kusalia uongozinikwa kumkaribia Kiongozi wa ODM Raila Odinga  kwa sababu anafahamu kwamba hali imekuwa moto Kitui .

“Ngilu anatafuta njia za kumkaribia Raila ili aweze kupata nafasi ya uongozi’

Muthama  amesema atamuunga mkono DP Ruto na watamfuata endapo atasalia Jubilee au ataondoka ili kuanzisha chama kingine .

Mwanasiasa huyo amesema hakuna anayeweza kutetea maslahi ya Ukambani kati ya Kalonzo na Ngilu

"Ngilu  hawezi kuongoza muungano thabiti .Mtu anayeweza kufanya hivyo kuiongoza Ukambani ni Kivutha’ amesema

Kivutha ametangaza kwamba atawania urais mwaka wa 2022  hatua inayomuweka katika nafasi nzuri ya kuanza kujadiliana na wengine kuhusu uwezekano wa kuunda muungano wa kisiasa .

View Comments