Polisi wameshauriwa kuzingatia mwongozo wa  mashtaka ulitolewa na DPP ili kupunguza kuwakamata watu wa makosa madogo madogo  na kuwarundika katika rumande ,amesema waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’I .

Matiang’i  amelalama kuhusu idadi ya juu ya watu wa makosa madogo katika seli  akisema hatua hyo sasa inaigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kuwashughulikia . Aliyasema hayo Jumanne wakati wa uzinduzi wa  mwongozo kuhusu mashtaka katika  taasisi ya mafunzo ya mashtaka ,Loresho .

Amesema jela na  rumande  zina watu wengi  ambao kesi zao zinaweza kusuluhishwa kwa haraka kupitia njia mbadala za kusuluhisha mizozo .

“ iwapo mwongozo huu utafatwa ,idadi ya  watu wa maosa madogo katika jela na rumande itapunguzwa’ amesema

Kwa mfano mtu anayekiuka sheria za trafiki  hulipa faini ya shilingi 600 ilhali kumweka rumande kutagharimu zaidi ya shilingi 30,000 .

Matiang’i  alisifu sana mwongozo huo akisema utazuia kuwekwa seli kwa watu ambao kesi zao zinaweza kushghulikiwa nje ya mahakama haraka na kuokoa pesa za serikali  kwalengo la kuhakikisha kwamba ni kesi zenye ushahidi na za kutafuta haki kwa walalamishi zinazopewa uzingativu .

Mwongozo huo unamhitaji mwendesha mashtaka kutathmini ubora wa usahhidi wake  kabla  ya kuamua kuendelea na kesi  mahakamani .

View Comments