Conjestina ana machungu sana kuhusu kutengwa na kutopokea usaidizi wowote na serikali-Carol Radull
Carol Radull hivi maajuzi alimtembelea mwanabobdia wa zamani wa Kenya Conjestina chien’. Ziara hiyo imefungua hisia nyingi kali huku wengi wakishuhudia jinsi usaliti unavyoweza kumpata gwiji yeyote amabaye anajituma kuiwakilisha nchi hii katika ulingo wowowte hasa katika sanaa na spoti .
Conjenstina alikuwa nyota wa Kenya na miaka ya 2000 aliwasha nyota ya Kenya katika ulingo wa ndondi kwa upande wa akina dada lakini hali yake imekuwa ikidorora bila hatua yoyote kuchukuliwa na maamlaka husika kuanzia kwa serikali hadi kwa wasimamizi wa michezo .
Mambo hayakuwa mazuri kwa staa huyo wa zamani wa ndondi na mara ya mwisho wakenya wengi walisikia kumhusu ni wakati gavana wa Nairobi Mike Sonko alipomtoa Siaya na kumpleka kwa matibabu mwaka wa 2019.
Radull alipiga picha kadha na Conje ambazo zinaonyesha taswira ya kuvunja moyo na alieleza jinsi Conje mwanzoni alivyokuwa na hasira walipokutana lakini akatulia baada ya wao kuzungumza kwa muda . Pia amesem kwamba mwanandondi huyo amepoteza uzani huku akionyesha kwamba bado anapenda sana medali alizoishindia kenya kwani amezihifadhi kwa njia nzuri .
Carol alisema kwamba Conje alihisi kuachwa na maamlaka husika za michezo katika wakati wake mgumu ambapo msaada kwake ungekuwa jambo la muhimu sana ili kuyabadilisha maisha yke .
Baada ya ujumbe huo wa Radull watu wengi na wahisani wamejitokeza wakitaka kumsaidia Conje lakini wasichofahamu watu ni kwamba Conje anahitaji makakati wa muda mrefu unaoweza kuhakikisha kwamba harejei tena katika mazingira mabyo yanamtia katika hatari ya kujitumbukiza katika utumizi wa dawa za kulevya na msongo wa mawazo bali anahitaji njia ya kuweza kuitumia talanta yake na kuhisi kuhudumia tena nchi yake .