pjimage

Tangu kuripotiwa kwa virusi vya corona  nchini,watu kadhaa wamepoteza maisha ya na kufikisha idadi ya walioangamia nchini kuwa 369.

Hii leo nimekuchorea taswiri ya watu maarufu nchini waliopoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo.

 Ken Ouko

Ouko alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi na alifariki akiwa na miaka 56 baada ya kuambukizwa virusi hivyo hatari .

Ouko alikuwa alikuwa mhadhiri wa Sosholojia na mchambuzi wa maswala ya kisolojia katika vituo mbali mbali vya runinga nchini.

Charles Bukeko

Ni muigizaji aliyekumbana na kifo chake muda mfupi tu alipokuwa amewasilishwa katika hospitali ya Karen Jijini Nairobi .

Shirandula kama alivyokuwa anafahamika kutokana na uigizaji wake kwenye kipindi cha Papa Shirandula alifariki akiwa na miaka 58 muda mfupi tu baada ya kukumbwa na shida ya kupumua,tatizo lililosababishwa na viruis vya Corona.

Doreen Adisa Lugalia

Mhudumu huyu wa afya na mama wa watoto wawili pacha alikumbana na gonjwa hili hatari akiwahudumia wakenya waliokuwa wamelazwa katika hospitali za humu nchini baada ya kuambukizwa maradhi hayo.

Lugalia ambaye alikuwa na miaka 38 aliaga dunia siku kadhaa baada kulaza katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi,akiwa mhudumu wa kwanza kuangamizwa na virusi hivyo nchini.

Kifo chake kiliibua hisia kinzani miongoni mwa wahudumu wengine baada ya kuibuka madai kuwa walikuwa wanafanyika kazi bila ya vifaa vya kuwaginga dhidi ya virusi hivyo.

Prof Maurice Kizito Mang'oli

Mwendazake Mang'oli alikuwa mhadhiri wa Uhandisi katika chuo kikuu cha Technical jijini Nairobi na alipoteza maisha yake baada ya kulazwa katika hospitali ya Nairobi kutokana na virusi hivyo.

Mang'oli alifariki akiwa na miaka 67 na alimiminiwa sifa na wenzake kama mtu alietekeleza wajibu wake kwa kujitolea kikamilifu.

Atakumbukwa pakubwa kwa kutoa ushauri kwa jengo kuu la City Hall Annex jijini Nairobi mwaka 1980.

Tony Waswa

Waswa jamaa wa miaka 48 na kakaye mbunge wa Westlandd Tim Wanyonyi na kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula alifariki ghafla mnamo Mei na baada ye kubainika kuwa alifariki kutokana na virusi hivyo.

Waswa alifariki akiwa anapokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi na siku chache baada ye kuzikwa katika boma lake eneo la Mukhweywa kaunti ya Bungoma.

Hadi wakati wa kifo chake alikuwa anahudumu katika afisa za CDF eneo la Westlands linaloongozwa na nduguye.

Isaach Cherogony

Mumewe mwakilishi wa wanawake wa kaunti ya Baringo Gladwel Cheruiyot alifariki muda mfupi tu baada ya kufikishwa katika hospitali kuu ya Eldoret mnamo Julai 4 kutokana na virusi hivyo.