- shusho 3
- shuhso 2
- shusho 1

Msanii wa gospel wa Tanzania Christina Shusho ametoa mtazamo tofauti kuhuu ndoa akisema wanawake wengi hutaka wanaume ambao wanaweza kuwatunza na kuwapa ulinzi kama walivyotunza na baba zao na sio  pesa au ngono tu .

Shusho  alielieza kwamba ingawaje kuna wanawake wanaovutia na pesa au  ngono ,wengi wanataka mwanamme wa kuwalinda vizuri kama walivyotunzwa na baba zao .

Shusho alikuwa akizungumza katika channel yake ya Youtube   ambapo ameeleza kwamba mwanamme anapotoka kwao kwenda kuolewa  basi mume wake anafaa kuchukua pia majukumu ya ‘ulezi kama baba’

“ Ziba pengo hilo pindi tu anapokuja kwako kama mkeo ili uchukue pia majukumu kama bba mlezi’ amesema

Msanii huyo wa kibao  “Unikumbuke”  amesema kwamba ndoa nyingi  huvunjika kwa ajili ya mwanamme kukosa ufahamu wa kutosha kuhusu vitu vingi . Christina mwenyewe aliachana na mume wake na kuondoka kanisa lake akisema Mungu alikuwa na mipango tofauti naye . Aliwahimiza wanawake kutoua ndoto zao kwa sababu ya  kuhitajika kuwafurahisha wanaume katika maisha yao .

Ameongeza kwamba wakati mwingine hatima za watu hazipo pamoja na kila mtu wakati mwingine lazima ajitafutie ufunuo wa kujua umuhimu wake

View Comments