- -Skk9kpTURBXy8xM2Q4MTk5NzI4YTIzOTM1NTkxYjM5MWY3M2VkNjIyNS5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
- IMG-20200807-WA0007
- Mutahi Kagwe
- Mutahi Kagwe

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ijumaa huku akitangaza maambukizi ya corona alisema kuwa kaunti zote,47 zimesajili visa vya maambukizi ya virusi vya corona.

Akiwa katika kaunti ya kisii alipokuwa amekaribisha na gavana wa kaunti hiyo James Ongwae, alitangaza habari hizo na kusema kuwa kaunti zote zinapaswa kuwa tayari kukabiliana na virusi hivyo.

"Kesi za maambukizi ya corona zikiendelea kuongezeka nchini itakuwa vigumu sana kujuwa na kufahamu kesi hizo za maambukizi ni za kaunti gani

Tunapaswa kuwa na uwezo wa kukabiliana na virusi vya corona." Alizungumza Mutahi.

Pia alikumbush wanachi kuwa kuna virusi ambavyo vinachukua maisha ya wananchi kila siku mbali na corona huku akiupa ugonjwa wa saratani kipaumbele na ambao umeathiri maisha ya wananchi sana.

Mutahi aliwaambia wananchi wasichoke kuenda hospitali kwa ajili ya uoga wao wa kuambukizwa virusi vya corona, wanapaswa kuenda na kupokea matibabu.

"Tumejua kuwa kunawagonjwa ambao hawatembelei mahospitali zetu kwa maana wanaogopa kuambukizwa virusi vya corona tumechukua hatua kuhakikisha vifaa vya corona vimetengwa na vifaa vya hospitali ya kawaida So msiogope, endeni hospitalini kama uko na ugonjwa."

View Comments