pjimage (7)

OCS  wa kituo cha polisi cha Boya huko Kisumu  chief inspector William Cheruiyot  ni miongoni mwa maafisa wa polisi waliokamatwa siku ya jumatatu kwa kuiba pombe .

Afisa huyo alikamatwa  pamoja na wado wake wanne  Jane Chepkemei (CP No. 83816), Bernard Macharia ( PC No.110581), Samuel Maina ( PC No.119196)  na  Rodrick Laushuset (PC No. 59664).

Ripoti ya polisi inaonyesha kwamba  walikamatwa baada ya kuiba pombe  ya White  Pearl  Vodka kutoka kwa lori ambalo lilipata ajali wakati lilipokuwa likisafirisha pombe hiyo . Ajali hiyo iliyohusisha lori la Isuzu  KCK 959L  haikusababisha majeraha ya waliokuwemo .

Polisi hao wanadaiwa kuiba pombe hiyo badala ya kuilinda  na baadaye chupa 72 za kileo hicho zilipatikana katika nyumba ya OCS Cheruiyot .

Tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Ahero  ,kaunti ndogo ya Nyando  kupitia   nambari ya OB  OB3/10/08/2020  NA  41/10/2020.

OCS  huyo alizuiliwa katika kituo cha polisi cha  Kisumu Central .

View Comments