Serikali au Upinzani? Karua amkosoa Raila Kuhusu wajibu wa upinzani
Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amemkosoa kiongozi wa ODM Rila Odinga kuhusu matashi yake kwamba upinzani upo ndani ya serikali
Raila siku ya alhamisi alidai kwamba chama cha ODM Kipo upinzani na pia serikalini . lakini karua ametumia mitandao ya kijamii kukosoa hilo akisema
" Ni mkanganyiko wa maksudi! Katiba inaeleza kuwepo kwa chama tawala kilicho serikalini na chama cha upinzani katika kiwango cha kitaifa na pia katika kaunti . kujifanfa kwamba upo ndani ya serikali nan je kama upinzani ni ukiukaji wa katiba !’ amesema Karua
Karua amesema upinzani sasa ndio unaozungumza kwa niaba ya serikali .
"... tunazungumza kuhusu ukosefu kabisa wa uangalizi na wanachama cha chama cha wachache sasa wanazungumza kwa niaba ya serikali’ amesema Karua
Raila katika hotuba yake siku ya alhamisi alipuuza madai kwamba mwafaka wa handshake kati yake na rais Kenyatta umelegeza nguvu za upinzani .
Amesema sio jambo sawa kukitaraji chama cha ODM kuwa ndicho cha kuikosoa serikali .
" vyomvo vyetu vya habari havina ufahamu wa kutosha kuhusu wajibu wa chama cha ODM . kabla ya katiba mpya tulikuwa na mfumo wa mseto wa bunge na rais ambapo upinzani uliangalia oparesheni za serikali .katika mfumo wa sasa wa urais ambapo kuna serikali ,bunge na idara ya mahakama ,mambo ni tofauti’ Raila alisema
Raila amesema ni jukumu la bunge kuangalia shughuli za serikali kwa ushirikiano na chama cha walio wachache na sio jukumu la upinzani pekee