mdv

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amepuuzilia mbali mjadala wa 'hustler' na 'dynasty', akisema kwamba hali ya mtu haifai kutumika kama chambo katika mashindano ya kisiasa.

Wandani wa naibu rais William Ruto wamekuwa wakisema kwamba wanasiasa kutoka familia maarufu 'dynasties' zimekuwa zikiweka mikakati ya kumzuia Ruto kuwa rais wakisema kwamba sio hatia kwa mtu maskini 'hustler' kama yeye kupanda kufikia kiwango cha kuwa rais.

Soma habari zaidi;

Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odingwa wamekuwa wakisemekana kutoka familia mashuhuri 'dynasties' kwa sababu wao ni wana wa aliyekuwa rais wa kwanza wa Kenya na makamu wa kwanza mtawalia.

Soma habari zaidi;

Hata hivyo, Mudavadi alisema mjadala huo: "Ni upumbavu na unalenga kugawanya... Ni kama kulinganisha watu wanaoamini Mungu na wale ambao hawaamini uwepo wa Mungu. Umaskini sio jambo la kujivunia."

"Wacha tujadiliane kama 'sera zangu zitawezesha kubuniwa kwa nafasi za kazi au la... je zitaondoa ufisadi au la; zitaimarisha huduma za afya au la..."

Akiongea katika mahojiana kwa NTV siku ya Alhamisi, Mudavadi alisema kwamba umaskini haufai kuonekana kama hali ya kuishi nayo milele.

Alipuuzilia mbali dhana kwamba yeye anatoka kwenye familia ya 'dynasty'.

"Babangu alizaliwa Magharibi mwa Kenya; babake alifariki katika mgodi wa dhahabu akichimba... akijitafutia, alizikwa hapo. Alikuwa maskini," Mudavadi alisema.

Alisema kwamba hatahusishwa katika mjadala ambao hauna msingi ila kugawanya taifa kwa misingi ya 'husler' na 'danasty'.

View Comments