- William Ruto
- Raila Odinga

Naibu Rais William Ruto ameunga mkono hatua ya kuunda kamati ya seneti ili kusuluhisha mjadala wa ugavi wa fedha ambao unaonekana kukumbwa na utata si haba.

Ruto alisema itakuwa jukumu la kamati hiyo kutumia busara ya hali ya juu katika kuamua njia mwafaka itakayotumika baada ya maseneta kufeli kuafikiana katika vikao walivyofanya mara tisa.

Wakati uo huo alikashifu vikali dhuluma dhidi ya viongozi wenye maoni kinzani akisema kuwa wananchi hawakuipigia kura serikali ya Jubilee ili kunyanyaswa.

"Hatua ya kuwatishia wananchi, kuwanyanyasa na kuwadhukumu viongozi ni makosa, na hiyo sio sababu iliyowafanya mamilioni ya wananchi kurauka kutupigia kura." Ruto Alisema.

Watatu hao walikamatwa wakiwa maeneo tofauti kaunti za Nairobi na Kajiado katika njia isiyoeleweka. Watatu hao walikuwa miongoni mwa viongozi waliopinga pendekezo la serikali kwamba fedha za baadhi za kaunti zipunguzwe.

Aidha kinara wa Upinzani Raila Odinga pia alikashifu kukamatwa kwa maseneta hao na kudokeza kwamba hatua hiyo iligihirisha Kenya ingali katika enzi za ukoloni.

“Kukamatwa kwa maseneta hao jana, kama vile mzozo wa kuhusu mswada wa ugavi mapato, ni dhihirisho kuwa hatujaafikia demokrasia."
View Comments