‘Jubilee ni kama karatasi, tutaitupa’ asema Oscar Sudi
Naibu wa rais William Ruto na kambi yake huenda wanasalimu amri katika vita vya kukipigania chama cha Jubilee ambacho awali alilenga kukitumia kuwania urais mwaka wa 2022 .
Washirika wake wamesema walilenga kuiunganisha mirengo ya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu ujao lakini kwa sababu kimetekwa na ‘walaghai na mabroka’ hivi karibuni watatoa mwelekeo kwa wafuasi wao .
Hayo yamesema na mbunge Oscar Sudi ambaye amesema Ruto ana chaguo mbadala kuhusu chama atakachotumiwa kugombea urais .
" Kama alivyosema bosi , tutajaribu kusuluhisha tofauti hizi lakini tuna njia nyingine mbadala. Jubilee ni karatasi tu na tutaibuka na karatasi nyingine wakati ufaao’ Sudi amesema
" Hata iwapo Ruto atawania urais kwa chama kiitwacho Sufuria basi hapo ndipo tutakapoelekea’
Hata hivyo sudi amesema hatawakiacha Chama hicho bila kuwatoshoa kijasho wapinzani wao .
Sudi alikuwa akizungumza nyumbani kwake Eldoret ambako alikuwa mwenyeji wa Zaidi ya waakilishi 69 wa kaunti kutoka Uasin Gishu, Nandi na Trans Nzoia kwa chakula cha mchana na kujadili masuala ya eneo hilo.
Sudi amedai kwamba janga la covid 19 limeingizwa siasa ili kuwazuia wafuasi wa Ruto kukongamana .
“ Nimekuwa nikizingumza kuhusu mambo mengi likiwemo jambo hili feki la Covid 19 na hivi karibuni nitajitokeza kutabiri kitakachofanyika siku chache zijazo’ amesema Sudi
Sudi ameahidi kulipasha taifa kuhusu mwelekeo utakaochukuliwa na wafuasi wa DP Ruto .
Sudi alitangaza kwamba tazidi kuandaa hafla za mikutano na waakilishi wa kaunti kutoka Baringo, West Pokot, Nakuru na maeneo mengine .