Siku chache baada ya kinara wa ODM Raila Odinga kumsuta seneta Cleophas Malala, Jumapili kwa kupinga mfumo mpya wa ugavi wa mapato hatimaye ameweza kumtembelea kinara huyo afisini mwake Capitol Hill.

Raila alishangazwa endapo Malala alichaguliwa kuwakilisha watu wa Kakamega baada ya kupinga mfumo huo, huku akimsuta Seneta huyo Raila alikuwa na haya ya kusema,

"Endapo umechaguliwa kama mbunge ama seneta,unatakiwa kuwakilisha watu. Mfumo umewasilishwa Seneti lakini unasema hautaki kuwanyima watu wa kaunti zingine pesa, umechaguliwa kweli na watu wa Kakamega?

Endapo kuna seneta ambaye kaunti yake inapokea pesa nyingi lakini anapinga mfumo huo sio eti anawapenda watu wa kaunti zingine, kuna shaka." Alizungumza Raila.

Ni ugavi wa mapato ambao unaungwa mkono na baadhi ya maseneta huku wengi wakiupinga, baada ya kuwa na mkutano na kinara huyo Malala alisema kwamba,

"Nimechangamka kwa kuwa na mazungumzo na mheshimiwa Raila Odinga kuhusu mkazo unakabili ugavi wa mapato katika seneti, tulipata kuwa ugavi wa mapato ya shillingi moja mwananchi mmoja inasaidia kaunti zote ili kuweka utulivu wa nchi yetu

Nilimhakikishia kinara Raila Odinga kuwa mimi na wenzangu tutajadili kuhusu ugavi huo kwenye seneti."

Seneta imeahirisha kikao chao cha ugavi wa mapato zaidi ya mara tatu kwa kutosikizana kwa maseneta.

View Comments