Tume ya uwiano na utangamano imezua wasis wasi kuhusu matamshiya mbunge wa Kapseret Oscar Sudi kumhusu rais Uhuru kenyatta na familia yake .

NCIC imewashauri wakenya kudumisha utulivu  na uvumilivu wakati mashirikahusika ya serikali yanapochunguza suala hilo . Sudi siku ya jumatatu alijitokeza akwa maneno makali alipokuwa akimtetea mbunge wa Emurua Dikiir Johanna Ng'eno  aliyekamatwa pia kwa kumzungumzia raisUhuru kenyatta na na mamake rais Mama Ngina Kenyatta .

Polisi huko Transmara Mashariki walimkamata Ng'eno  kwa matamshi yake  ya uchochezi dhidi ya  rais Uhuru kenyatta nafamiliayake .

Akikubaliana na Nge'no  Sudi alilalamika kuhusu hatua ya rais kenyatta kumtenga naibu wake licha ya kumsaidia kushinda uchaguzi mara mbili .

“ Nataka kumuambia rais  kwamba hatuna deni lake ,tulikupigia kura mara tatu -mwaka wa 2013 na 2017 mara mbili ..nchi hii ni yetu sote' Sudi aliyekuwa nahamaki amesema

 aliongeza kusema kwamba rais kenyatta amemsaliti naibu wake William Ruto  na ameonekana kumtenga katika serikalialiosaidia kuunda . Matamshi yake hata hivyo yamekosolewa hata  na Naibu wa rais mwenyewe  .Ruto amesema viongoziwanafaa kuishemu afisi ya  rais na rasi Uhuru kenyatta