Uhuru anapaswa kuita kamati ya bunge,' Hisia za Wakenya baada ya usemi wa Oscar Sudi
Baada ya mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi kutoa matamshi yake ya kumsuta rais Na familia wakenya wengi walitoa hisia tofauti kuhusu matamshi ya mbunge huyo.
Sudi alikuwa akizungumzia kukamatwa kwa mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng’eno aliyekamatwa siku ya Jumatatu alasiri kuhusiana na madai ya kutoa matamshi ya chuki na kudhihaki rais Kenyatta.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sudi alisema ya kwamba akina mama wote wanapaswa kupewa heshima.
Hii ni baada ya naibu rais Ruto kujitenga na matamshi ya Sudi na Johana Ng'eno.
"Kwa kutoa ufafanuzi hapa, si kumtusi mama ya mtu nilirudia kwamba mama yangu,mama Ngina na akina mama wote wanstahili kupewa heshimaHata hivyo mwenzangu Johana Ng'eno alikamatwa kwa kutaja jina lake mama Ngina, hamna mama wa mtu ambaye ni muhimu kuliko wa mwingine
Hayo ndio maoni yangu." Aliandika Sudi.
Ni ujumbe ambao uliibua hisia mseto na hata mjadala kwenye mitandao hiyo na hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya;