Shirika la Kemsa limetajwa tena katika sakata ya shilingi bilioni 63 ya ununuzi wa mashine ya matibabu huku tume ya EACC Ikiendelea kuchunguza  wizi wa fedha  za Covid 19 katika shirika hilo .

Ripoti moja ya senate  imeihusisha kemsa na  kupotea kwa fedha katika mpango huo wa ununuzi wa  mitambo ya hospitali kwa jina MES

Ufichuzi huo unalitia shirika hilo katika shinikizo Zaidi hasa wakati huu ambapo EACC inaendelea na uchunguzi mwingine kuhusu jinsi kemsa ilivyotumia mabilioni ya pesa za Covid 19 ili kununua vifaa vya kupambana na janga hilo .

Mameneja wa shirika hilo wakiongozwa na Afisa mkuu mtendaji Jonah Manjari aliyesimamishwa kazi  walieleza jinsi walivyotoa  kandarasi za mamilioni ya pesa kwa kampuni ambazo hazikustahili kupewa zabuni hizo na kukiuka sharia za uagizaji wa bidhaa .

Katika ripoti hiyo ya senate Kemsa inashtumiwa kwa kujipa  jukumu la kuzichagua kampuni ambazo  uwezo wake unatiliwa shaka kutoa mashine   na vifaa vya matibabu  vilivyohitajika chini ya mpango wa MES

Kemsa   haikubaini iwapo vifaa na kemikali hizo zingeweza kununuliwa kutoka kwa kampuni nyingine kwa gharama ya chini .

View Comments