Walinzi watatu waliojihami wa rais ni miongoni mwa wale waliokamatwa, polisi walipovamia nyumba ya mbunge wa Kapseret Oscar Sudi kumkamata ili afikishwe mahakamani kwa mashtaka ya kutamka matamshi ya chuki na uchochezi.

Kamanda wa polisi wa Uasin Gishu Johnstone Ipara anasema afisa mmoja na mlinzi wa sudi walijeruhiwa katika vurugu hiyo. Aidha, Wakili wake Sudi na seneta Kipchumba Murkomen wamesema kuwa watamsindikiza kujisalimisha kwa afisi za tume ya uwiano na utangamano.

Hayo yakijiri, polisi katika kaunti ya Bomet wameanzisha msako wa wanaume watano wanaodaiwa kuwateka nyara ndugu wawili waliokuwa wakihudumu katika maduka tofauti ya Mpesa katika eneo la biashara la Ngariet.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo Naomi Ichami anasema washukiwa hao wanadaiwa kujifanya  walikuwa wantaka kuweka shilingi elfu 40 kwenye simu ambapo walijiingiza katika maduka hayo na kuwatia pingu ndugu hao  kabla ya kuwaingiza katika gari moja. Inasemekana gari hiyo iliondoka upesi kupitia njia ya Sotik.

Kwingineko, mbunge wa Kesses Swarrup Mishra amewataka viongozi kukomesha migogoro kati ya vyama vya kisiasa inayohujumu maendeleo humu nchini. Mishra anasema viongozi wa chama tawala wanastahili kujikita katika kuwahudumia wananchi badala ya kupiga siasa za uchaguzi wa mwaka 2022. Aidha, mbunge huyo anasema anasalia kuwa mwanachama wa Jubilee lakini hatashawishiwa wala  kulazimishwa na yeyote kuchukua upande mmoja kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake

View Comments