Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi atafikishwa katika mahakama ya Nakuru leo baada ya kujisalimisha kwa polisi siku ya jumamosi huko Eldoret .

Sudi anatarajiwa kujibu mashtaka ya uchochezi  kuhusu matamshi yake  ambayo yamelaaniwa na viongozi mbali mbali na alikuwa akisakwa na polisi kabla ya kujisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi cha Langas Eldoret .

Alikamatwa na polisi ambao baadaye walimsafirisha kwa helikopta hadi Nakuru .kundi la mawakili wake likiongozwa na  Gladys Shollei linasisitiza kwamba  mbunge huyo hakutamka neno lolote la uchochezi na wako tayari kumtetea mahakamani .

Sudi  anashtumiwa kwa kutoa matamshi makali dhidi ya  rais Kenyatta na  mamake rais , mama Ngina Kenyatta .

View Comments