Oscar Sudi kusalia seli kwa siku mbili
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi atasalia korokoroni kwa siku mbili akingja uamuzi kutolewa kuhusu ombi lake la kuachiliwa huru kwa dhamana .
Alifikishwa mbele ya hakimu mkuu wa nakuru Josephat Kalu ambapo upande wa mashtaka ulitaka kuruhusiwa kumzuilia kwa siku 14 ili kutoa fursa ya uchunguzi kufanywa .
Hakujibu mashtaka dhidi yake iwangawaje serikali inapanga kumshtaki kwa makosa matano ya uchochezi na kutoa matamshi ya kuzua chuki ,kumshambulia afisa wa polisi , mienendo isiofaa,Kukataa kukamatwa na kumiliki bunduki kinyume cha sheria .
Sudi alijisalimisha kwa polisi siku ya jumamosi huko Eldoret baada ya polisi kumsaka kwa Zaidi ya saa 48 na baadaye alisafirishwa kwa helikopta hadi Nakuru . Mbunge huyo ameshtumiw kwa kutoa matamshi makali dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na mama wa kwanza wa taifa Mama Ngina Kenyatta .