- Korane 2
- Korane 1

Gavana wa Garissa Ali Korane ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.25 pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni tano .

Korane  pia amezuiwa dhidi ya kwendaafisini mwake a kuagizwa kuiwasilisha paspoti yake mahakamani .

Gavana huyo jumanne alishtakiwa kwa ufisadi mbele ya mahakama ya  kupambana na rushwa ya milimani .

Anashtumiwa kwa kutumia vibaya shilingi milioni 233 kutoka kwa Benki ya dunia zilizofaa kusaidia mradi wa kuboresha Miji . ameshtakiwa pamoja na watu wengine wane kwa njama ya kutekeleza uhalifu wa kiuchumi na ulaghai .

Walikanusha mashtaka mbele ya hakimu mkuu Douglas Ogoti .

Akimuachiliwa kwa dhamana ,hakimu Ogoti  amesema hakukuwa shtaka la kupotea kwa pesa katika stakabadhi ya amshtaka  na Korane alikabiliwa shtaka jingine la kukataa kufuata shera za utumizi wa fedha za umma .

Upande wa mashtaka haukupinga kuachiliwa kwao kwa dhamana lakini ulitaka masharti makali ya dhamana kutolewa na jaji . Naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Alexander Muteti  aliitaka mahakama kumzuia gavana huyo na walioshtakiwa naye dhidi ya kwenda katika afisi zao .

View Comments