15 September 2020 1 Min Read
Geoffrey Majiwa aapishwa kama naibu spika wa bunge la Nairobi
by Yusuf Juma Habari
Aliyekuwa meya wa Nairobi na mwakilishi wa wadi ya Baba Dogo Geoffrey Majiwa amechaguliwa kuwa naibu spika wa bunge la kaunti ya Nairiobi
Alithibitishwa katika wadhifa huo na spika wa bunge hilo Benson Mutura wakati wa kikao cha jumanne alasiri . Spika huyo aliutangaza kwamba hapakuwa na mgombeaji mwingine aliyekuwa amewasilisha stakabadhi zake kwa wakati ufaao .
Ni mwakilishi wa wadi ya Ngei Redson Otieno alikuwa ameonyesha nia ya kutaka kiti hicho lakini hakuwasilisha stakabadhi zake .
Kiti hicho kilisalia wazi baada ya JohnKamangu kujizulu alhamisi wiki iliyopita .