Tanzania yaondoa marufuku dhdi ya kampuni za ndege za Kenya
Tanzania imeondoa marufuku dhidi ya safari za ndege za Kenya nchini humo siku moja tu baada ya Kenya kuwaruhusu raia wa Tanzania kuja Kenya bila kuhitajika kwenda karantini ya lazima ya siku 14 .
Kupitia taarifa iliyotolewa jumatano mkurugenzi mkuu wa maamlaka ya safari za ndege nchini Tanzania Hamza Johari amesema safari zote za ndege kutoka Kenya sasa zinaruhisiwa katika anga ya Tanzania .
Kenya siku ya jumanne iliamua kuiweka Tanzania katika rodha ya mataifa ambayo raia wake sio lazima wawekwe katika karantini ya siku 14 wanapowasili nchini . Mataifa mengine yaliwekwa katika orodha hiyo ni pamoja na Ghana, Nigeria na Sierra Leone.
Mwezi agosti Tanzania ilipiga marufuku shirika la Kenya Airways dhidi ya kwenda nchini humo na kuzidisha mgogoro kati ya nchi hizo mbili