1600767786068(1)

Mashabiki na wakenya wengi waliwapenda wakisoma habari pamoja lakini hali ya maisha haikuwakubalisha kukaa kwenye vyombo vya habari pamoja kwa muda bali wengi walitengana katika kazi hiyo ya uhanahabari licha ya kuwa marafiki wa karibu.

Hii hapa orodha ya wanahabari waliokuwa wanasoma habari pamoja lakini wakatengana kwa sababu moja au nyingine.

1.Lulu Hassan na Kanze Dena

Wanahabari hao wawili hakuwahi dhani kama watatengana katika kazi yao kwa maana walikuwa marafiki wa karibu saana huku kazi yao ikiwapendeza wengi sana

Kanze alipata kazi ikuluni huku ikimlazimu kuacha kazi yake ya uhanahabari huku Lulu naye akianza kusoma habari na mumewe Rashid Abdalla.

2.Andrew Kibe na Kamene Goro

Watangazaji hao wa redio ya kiss kutengana kwao kuliwashtua wengi hii ni baada ya Kibe kuwasilisha barua yake ya kuacha kazi mnamo juni 2020 huku nafasi yake ikichukuliwa na Jalang'o.

3.Janet Mbugua na Hussein Mohamed

wawili hao waliachana mwaka wa 2015 ambapo Mbugua alichukua fursa ya kuenda kujifungua na kutorudi tena huku akimuacha Hussein ambaye baadaye alitoka kwenye runinga ya Cirizen.

4.Kalekye Mumo na Shaffie Weru

Walikuwa wafanyakazi ambao walikuwa bora katika redio ambapo wengi waliwapenda,Kalekye alitoka mnamo mwaka wa 2016 huku Shaffie akimpata mtangazaji mwenzake Adelle Onyango.

5.Victoria Rubadiri na Larry Madowo

Wawili hao walikuwa wakifanya kazi katika runinga ya ntv, huku weni wakisema kuwa wamo kwenye uhusiano wa kimapenzi, huku madowo akitoka kwenye runinga hiyo na kuenda katika runinga ya BBC ambapo amekuwa akifanya makubwa.

Mwishowe Rubadiri alitoka pia na kujiunga na runinga ya citizen.

View Comments