- Ruto 1
- ruto 2
- ruto 3

Naibu wa rais William Ruto  siku ya alhamisi ameonekana kuchukua hatua nyingine kivyake kwa  kuandaa mkutano na mgombeaji huru wa kiti cha eneo bunge la msambweni baada ya chama cha Jubilee kujiondoa kutoak uchagzi huo na kutangaza kwamba kitamuunga mkono mgombeaji wa chama cha ODM .

Ruto amesema alitaka Jubilee kuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo na siku ya jumatano alionyesha masikitiko wkamba Jubilee imeamua kumuunga mkono mgombeaji wa ODM.

Siku ya alhamuisi Ruto alikutana na  gombeaji huru  Feisal Abdallah Bader  anayetaka kuichukua nafasi hiyo baada ya kifo cha  Suleiman Dori .

Kupitia Twitter Ruto alisema amekutana na mgombeaji huyo aliyeandamana na wabunge wengine wa pwani .

Waliokuwa katika mkutano huo ni wabunge

Athman Shariff (Lamu East), Mohammed Ali (Nyali), Owen Baya (Kilifi North), Khatib Mwashetani (Lunga Lunga) na  Aisha Jumwa (Malindi)

Sharlet Mariam,  aliyekihama cha ODM  alisababisha kizaazaa katika makao makuu ya Jubilee akitaka kupewa tiketi ya  chama hicho kugombea uchaguzi huo mdogo .

Ruto alimtambua Mariam na kusema iwapo ataitisha usaidizi wake kuwania kiti hicho kama mgombea huru  basi atakuwa tayari kumpiga jeki .

Seneta wa Nairobi Johnstone Sakaja  amesema sio kwa maslahi ya Jubilee kutokuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo mdogo .

Kwa sababu chama hakina mgombeaji basi wanachama wana uhuru wa kumuunga mkono wanayemtaka .Rais hatomfanyia kampeini mgombeaji yeyote’ amesema Sakaja .

View Comments