- Mengi kati ya mataifa ya frika yaliwataka watu wake wavae barakoa kuaznia mwanzoni mwa mlipuko
- COVID
- Serikali za Afrika ziliwataka watu wavae barakoa mwanzoni mwa mlipuko
- Hospitali chache sana Afrika Kusini zililemewa na wingi wa wagonjwa wa Covid-19

Mkuu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (ECDC) ameyasifu mataifa ya Afrika kwa kuweza kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Afrika imeshuhudia maambukizi ya corona ya watu milioni 1.4, na vifo 34,000 tangu mwezi wa Machi.

Idadi hiyo ni ndogo sana kuliko ile ya mabara ya Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini na Amerika Kusini, huku idadi ya maambukizi ikiendelea kupungua.

Uingiliaji kati wa awali ulikuwa na mchango mkubwa katika kukabiliana na kusambaa , John Nkengasong amekiambia kipindi cha BBC Newsday.

Bara lenye watu zaidi ya bilioni moja limekuwa na chini ya 5% ya maambukizi ya virusi vya corona kote duniani na 3.6% ya vifo.

Dkt. Nkengasong ameyaelezea kama "uongo" madai kwamba idadi ya watu walioambukizwa virusi na vifo katika bara la Afrika haikuripotiwa ipasavyo.

" Huenda hatukubaini visa vyote, sawa na maeneo mengine ya dunia...lakini hatuwaoni watu katika maeneo ya bara wakiugua na kufa mitaani au mazishi ya watu wengi yakiendelea ," Dkt Nkengasong amesema.

Mataifa yote ya Afrika yalianzisha misururu ya hatua za kukabiliana na virusi mara tu mtu wa kwanza aliporipotiwa kuwa na virusi mwezi Machi.

Katika nchi nyingi , ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, zilianzisha vipindi vya kukaa nyumbani, lakini nyingine kama vile Ethiopia zilichagua kuweka sheria kidogo.

Dkt. Nkengasong, hatahivyo, anasema sababu ya kuwa na idadi ndogo ya maambukizi ni "juhudi za pamoja za bara ", ambazo zililenga juu ya "kuongeza idadi ya watu wanaopimwa na kufuatilia watu waliokutana na waliopata maambukizi- (contact tracing) na la muhimu zaidi watu walivaa barakoa".

Onyo juu ya uwezekano wa wimbi la pili

Kushuka kwa idadi ya maambukizi ya Covid-19 barani zaidi ni kutokana na kupungua kwa maambukizi hayo katika nchi ya Afrika Ksuini, ambako kulikuwa na karibu nusu ya maambukizi yote kwa ujumla ya barani Afrika c

Kufikia Jumanne, Afrika Kusini ilikuwa imewapima watu zaidi ya milioni . Ukilinganisha na bara zima la nchi zaidi ya 50 ambapo watu milioni 10 walikuwa wamepimwa mwezi mmoja uliopita.

Kwa viwango vya kimataifa , hii ni idadi ya chini, na inatokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kupima na ukosefu wa wazalishaji wake katika Afrika . Hili linaendelea kushusha "mafanikio " ya Afrika katika kukabiliana na virusi.

Wakati kunaweza kuwa na visa ambavyo havikubainika, wataalamu kama Dkt. Nkengasong wanasema hakuna lolote linaloashiria kuwepo kwa vifo visivyoelezeka katika nyingi miongoni mwa nchi za Afrika.

Lakini kuna onyo kuwa kunaweza kuwa na wimbi la pili la maambukizi wakati nchi zaidi zinalegeza sheria za udhibiti wa maambukizi.

View Comments