Watu  218  wamepatikana na virusi vya corona  baada ya sampuli 5,424 kupimw akatika saa 24 zilizopita  na kufikisha jumla ya visa hivyo hadi kufikia sasa kuwa 37,707.

Idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 532,729. Visa vyote ni vya wakenya  isipokuwa vinane.159 ni wauame ilhali  59  ni wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini sana  ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 78 .

Nairobi ndio inayoongoza kwa visa 68  ikifuatwa na  Kisii  28,Mombasa 21,Kisumu 19,Kimbu 13  Kajiado 11,Busia 10,Machakos 8,Tharaka Nithi 6 ,Garissa 6, Taita taveta visa 5  Nakuru visa  4 ,Uasin Gishu visa 3,Narok visa 2,Laikipia visa 2 Kakamega visa 2,Kericho visa 2, Murang’a,Bomet,Kilifi  ,Migori ,nyandarua na Nyeri zina kisa 1 kila moja.

 Watu 170 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 24,504 idadi ya wote waliopona corona nchini hadi kufikia sasa .

Leo watu 13 wameaga dunia na kufikisha 682 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo .

 

View Comments