bangi

Watu watano wamekamatwa na bangi yenye thamani ya mamilioni ya shiolingi .

Bangi hiyo ilinaswa katika boma la  Martin Mungai katika eneo la  Mwireri Area, Juja Farm.

Mungai  alimatwa pamoja na  Henry Shakira, Musa Abdi, Abdi Matayo  na Brian Mwanzia  siku ya ijumaa usiku

Kunaswa kwa bangi hiyo kulijiri baada ya kupatikana kwa shamba la mmea huyo katika boma hilo .

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti  amesema watano hao walijaribu kumhonga afisa mmoja mkuu wa polisi shilingi  689,000 ili  waachiliwe huru .

Pesa hizo na dawa hizo za kulevya vimehifadhiwa kama ushahidi  kabla ya washukiwa kufikishwa kortini .

Wiki jana seneta wa Narok  Ledama Ole Kina alishauri kurekebishwa kwa sheria ili kuhalalisha utumizi wa bangi nchini kwa sababu za kimatibabu .

Seneta huyo aliisambaza viedo yake mtandaoni akiwa katika shamba la bangi nchini Lithuania .

 

View Comments