cashy

Taarifa ya Elizabeth Ngigi

Aliyekuwa mpenzi wa mwanamziki Khaligraph Jones, Cashy Karimi amemshutumu msanii huyo kwa kutogharamia mahitaji ya mwanawe.

Siku ya Jumapili aliandika kwa twitter; "@Khaligraph excuse me, your son is sick. Health insurance?" (@Khaligraph tafadhali, mtoto wako ni mgonjwa. Bima ya afya?).

Shambiki mmoja hata hivyo alijibu akimwambia ajukumikiye mwanawe. "Isn’t he your son, kwani? Take him to the hospital." (Si mtoto wako kwani, mpeleke hospitalini).

Cashy alijibu akisema kwamba, "Ni wangu, na pia ni mtoto wake. Nimempeleka hospitalini tangu nikiwa mja mzito sasa ana umri wa miaka miwili na nililipa, na risiti ambazo nimewasilisha kwa mawakili wangu na wake," alisema.

"Wazazi husaidiana, lakini hata sheria inafahamu mpaka wa mzaha unafikia wapi."

Wasanii hao wawili walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa takriban miaka sita na kuachana mwaka 2018.

Miezi michache baadye mwaka 2018, alijifungua mtoto wa kiume.

Katika mahojiano ya awali, Cashy alisema kwamnba alikatiza uhusiano huo kwa sababu haukuwa unamfaa lakini akasema kwamba hakuwa na 'mpango wa kando'.

Katika mahojiano na Mpasho, alisema kwamba mwanawe amekuwa mgonjwa kwa majuma mawili lakini Khaligraph hajajitokeza.

"Nimekuwa nikiwasiliana naye kupitia mawakili wetu lakini anaonekana kuchukulia suala lhili kwa mzaha," alisema.

"Kile nataka ni yeye kugharamia bima ya afya ya mwanawe. Nimekuwa nikijaribu kumfikia kwa mwaka lakini hajakuwa akinijibu. Anajua mtoto wake ni mgonjwa lakini hajachukuwa hatua yoyote".

Kupitia mtandao wa Intagram, Cashy pia aliweka picha za nyaraka ambazo mawakili wake walimtumia Khaligraph, anayedaiwa kuwa baba wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili akimtaka kuchukuwa majukumu ya uzazi.

Kisha aliwapongeza akina mama kwa kuwa watu spesheli katika maisha ya mtoto.

Jaribio la meza ya habari ya Word Is kumfikia Khaligraph liligonga mwamba kwani alikata simu. Pia hakujibu jumbe za simu alizotumiwa kuzungumzia madai haya.

Soma habari zaidi hapa;

View Comments