Ushauri wa Jaji mkuu David Maraga kwa rais Uhuru Kenyatta  kwamba alivunje bunge kwa sababu ya kutotekelezwa kwa kanuni ya usawa wa kijinsia limewaghadhabisha baadhi ya viongozi.

  Wabunge wengi wanasema hawapo tayari kwa uchaguzi na wamemkemea sana Maraga akisema anatishia kulitumbukiza taifa katika mgogoro wa kikatiba ,je wabunge wana sababu tosha kupinga hatua hiyo ama wanatetea kazi zao? .Sikiliza podi nzima kuhusu suala hili