Hii leo watu 115 wamepona virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 25,023 ya watu waliopona corona tangu kisa cha kwanza kuripotiwa na kurekodiwa humu nchini.

Huku hayo yakijiri pia watu 184 wamepatikana na corona na kufikisha idadi jumla ya 38,713 ya watu walioambukizwa corona hii ni baada ya ya sampuli 4,700 zilizopimwa ndani ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya 170 ni wakenya huku 14 wakiwa ni raia wa kigeni, pia 110 ni wanaume ilhali 74 ni wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi miwili huku mwenye umri wa juu ana miaka 88 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Vile vile watu 7 wamepoteza maisha yao na kufikisha jumla idadi ya 718 ya watu walioaga kutokana na corona.

View Comments