In Summary

 • Sikuweza kulipia omena kwa maana sikuwa na pesa nilitegemewa nyumbani kwa maana mume wangu alipoteza kazi.

 • Naomba msamaha kwa maana ulinilea kama mtoto wako, sikuwa na ubaya.

Gidi na Ghost zawadi
Image: Radiojambo

Katika kipindi cha patanisho leo mama Charity alituma ujumbe ili apatanishwe na rafiki yake ambaye muuzaji wa samaki aina ya omena baada ya kukosa kumlipa.

Ni tukio ambalo lilitokea wakati huu wa janga la corona, huku akieleza usimulizi wake alikuwa na haya ya kusema.

"Nataka nipatanishwe na Jane ambaye amekuwa akiniuzia omena na ninaenda kuuza lakini sikuweza kumrudishia pesa zake ambazo ni elfu tano.

 
 
 

Ni wakati ambao corona iliingia humu nchini alafu mume wangu akapoteza kazi kwa hivyo ni mimi nilikuwa nategemewa nyumbani.

Nataka tupatanishwe kwa maana si kumlipa kwa kutaka lakini ni shida ambazo tumepitia wakati huu wa janga hili." Alieleza Mama Charity.

Jane alipopigiwa simu hakuwa na mamboo mengi bali alimuelewa mama Charity kwa hayo yote na kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema,

"Kesho kuja kazini kwa maana ulikuwa wafanya kazi vyema, vile ulinyamaza nilidhani kuwa umekuwa na kichwa ngumu lakini kuja na kitu kidogo uanze kazi."

(Mhariri Davis Ojiambo)

View Comments