In Summary
  • Mbunge wa malindi Aisha JUmwa kufanyiwa ukaguzi wa kiakili
  • Jumwa kusalia korokoroni hadi Alhamisi atakapofikishwa mahakamni na mshtakiwa mwenzake
Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa Mbunge Aisha Jumwa,

Mashtaka imeagikza mbunge wa Malindi Aisha Jumwa kufanyiwa ukaguzi wa kiakili kabla ya kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi ili kujibu mashtaka yanyomkabili ya mauaji.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter walitoa uamuzi huo Jumatatu Oktoba 19, huku ikisema mshtakiwa mwenzake ambaye ni mlinzi wake pia atafanyiwa ukaguzi wa kiakili.

Jumwa na Otieno wanakashifiwa kwa kumpiga risasi na kumuua jamaa wa mwakilishi wa wadi ya Ganda Reuben Katana Mwarume Oktoba 15, 2019 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo.

 

 

Wawili hao watazuiliwa katika kituo cha polisi cha Port wakisubiri kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi, Oktoba 22.

Huu hapa ujumbe wa uamuzi huo;

" Aisha Jumwa atazuiliwa katika kituo cha polisi cha Port akisubiri kufanyiwa ukaguzi wa kiakili katika hospitali ya Coast General Jumatano, Oktoba 21 kabla ya kufikishwa mahakamani Alhamisi, Oktoba 22 kujibu mashtaka yanayokabili ya mauaji." ILisoma Taarifa.

Mwendazake alipigwa risasi baada ya vurugu kuzuka kati ya wafuasi wa Jumwa na wale wa chama cha ODM.

View Comments