In Summary
  • Uhuru atapeana mwongozo wa BBI Raila asema
  • Hakuna mtu atakaye simamisha Reggae, muda wa maoumziko umekwisha BBI iko tayari kuanza

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema ya kwamba rais Uhuru kenyatta n yeye atakaye toa mwongozi wa BBI.

Alisema hayo akiwa kwenye sherehe ya Mashujaa, katika uwanja wa Gusii huku akisema hamna mtu yeyote atakaye si mamaisha Reggae.

"Ni wewe Uhuru utakaye sema tutakacho fanya baada ya hapa kwa maana hamna mtu atakaye simamisha reggae." Alisema Raila.

 

Pia kiongozi huyo alisema kuwa wachezaji wote wa BBI wamepokea maagizo watakayo fuata na 'massage' baada ya likizo  na wamo tayari kurudi uwanaani kuendeleza reggae.

"Tulikuwa tunaenda Nakuru lakini shetani ikaanguka kutoka huko juu reggae ikaenda kwa half time

Muda wa mapumziko umekwisha na wachezaji wote wamepokea 'Massagge na reggae iko tayari kuanza ni wewe rais utakaye tuonyesha mahali tutaenda baada ya hapa

Tunapaswa kuangalia ni nini haswa kinakosekana nchini ili kuiendeleza mbele kama vile mababu zetu walitazama."

Usemi wake uliweka mambo wazi kuwa mpira uko mikononi mwa rais ili kutoa ripoti ya BBI.

View Comments