In Summary
  • Mambo ni pole pole Uhuru amwambia William Ruto
  • Ndugu yangu amepinduka ameanza kukimbia nyuma
  • Alinisaidia kuchagua wazee wa BBI ambao nimewatambulisha hapa

Rais Uhuru Kenyatta akihotubia wananchi wakati wa uzinduzi rasmi wa ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI) alifichua mambo kadha wa kadha kati yake na naibu wake William Ruto.

Huku akizungumza wakati wa uzinduzi wa BBI mnamo Jumatatu Rais alimshukuru naibu wake kwa kuwa naye katika safari hiyo ya BBI.

"Pia nataka kumshukuru naibu wangu kwa maana kwa muda huo wote nilimjulisha nini haswa kilichokuwa kinatendeka na alikuwa mmoja wa sehemu ya mchakato huo

Ukweli ni kuwa alinisaidia kuteua wazee ambao nimewatambulisha hapa,na nilimuambia kuwa vile nilifanya na mheshimiwa Raila Odinga BBI haikuwa ya kuzingatia yatakayo tendeka mnamo mwaka wa 2022, mbali zaidi ya yale tulitenda pamoja mwaka wa 2013

ili tuweze kuleta kila mmoja katika bodi na kuhakikisha hamna mkenya yeyote ameachwa nyuma." Alizungumza Uhuru.

Huku akizungumzia msimamo wake Ruto dhidi ya BBI alisema kwamba,

"Tulisonga pamoja, hapa katikati ndio 2022 ilianza kuleta shida akasahau yale mengine na ndio nasema tutulize boli, haya bado yatakuja. Miaka hairudi nyuma... Race ni ile ya relay, unakimbia na yule ambaye anafaa kupokea anakungojea mahali anfaa kuwa ndio ashike aendelee.

"Lakini my brother William hapa amepinduka ameanza kukimbia nyuma."

 

View Comments