In Summary
  • Murkomen ataka akaunti ya twitter ya ikulu kufungwa
  • Rais alisema hakuna jambo la maana kwenye mitandao ya kijamii ni matusi tu/
qiPJWXQt_400x400

Matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusu mtandao wa Twitter wakati wa kuzinduliwa kwa shughuli ya ukusanyaji sahihi za BBI yanazidi kuibua hisia mseto.

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amehoji sababu ya Ikulu ya rais kumiliki akaunti ya Twitter ilhali Rais alisema 'huko ni matusi tu'.

"Rais alisema vizuri kuwa mitandao haswa Twitter ni bure na matusi tu ilhali kuna mtu angali afisini akifanya kazi kwenye @StateHouse Kenya.

 
 

Ni nani huyo ambaye anakosa kutii kiongozi wa nchi (kwa kuendelea kusimamia akaunti ya Twitter ya Ikulu?" Aliandika Murkomen.

Matashi yake Murkomen yanajiri saa chache baada ya rais kusema kwamba alitoka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuona hamna kitu chochote ambacho kinaedelea huko.

Rais alizungumza haya Jumatano siku ya kuzindua kwa mchakato wa ukusanyaji saini za BBI.

“Mimi sio mtu wa hiyo (social media). Ata Twitter niliondoka huko nikaona hii kitu ni bure ni matusi tu hakuna kitu inaendelea huko. Unakaa hapo unasoma, hulali ... unakaa hapo ukiangalia eti huyu amesema nini huyu hivi unachukua simu unaanza kupiga eti unaona huyu amenitusi . Afadhali nipige story na mama, nilale, niamke, niende kazi na dunia iendelee." Rais Alisema.

Baada ya wanamitandao kuona ujumbe wake Murkomen waliibua hisia mseto na walikuwa na haya ya kusema;

ISPAN KIMUTAI: Face with tears of joyFace with tears of joyFace with tears of joy Atasema alisoma kwa magazeti kuwa kuna Twitter account ya State House

Highland Ostrich: Mtu aniulizie kama gazeti iliacha kufunga nyama.

 

William Chepkut: He said that on a personal level. @StateHouseKenya is a state account for the office of the President. @NziokaWaita

Jerry KIm: So meaning that whatever is posted there is done without the awareness of the president? So what's the relevance of its existence?

kingston kushiki: Boss that account communicates the events of that office.. it doesn't need his approval

(Mhariri Davis Ojiambo)

 

View Comments