In Summary
  • Margaret kupeperusha bendera ya UDA katika kinyang'anyiro cha uaniaji kiti cha ugavana Nairobi
  • Chama hicho kilisajiliwa rasmi Ijumaa 8 Januari 2021

Chama cha United Democratic Alliance – kinachohuisishwa na naibu rais Willaim Ruto kimesajiliwa rasmi.

Hii ni ishara  tosha kwamba Ruto anaweka mikakati akijiandaa kukihama chama tawala cha Jubilee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Katika uchaguzi mdogo wa ugavana kaunti ya Nairobi Askofu Margaret atawania kiti hicho kupitia kwa tiketi ya chama hicho.

 

Msajili mkuu wa vyama vya kisiasa Anne Nderitu alithibitisha kubadilishwa kwa jina la chama cha Party of Development and Reform (PDR) hadi UDA.

Alex Kanya naye atapeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo ya Matungu uku Evans Kakai akipeperusha katika wadi ya Kabuchai.

Muthama akizungumza kwa ajili ya chama hicho alisema kwamba chama hicho kinaweza waleta wakenya pamoja.

Pia Murkomen alidai kwamba wako tayari kupambana na mashindano kutoka kwa vyama vingine vya kisiasa.

"Hatuogopi mashindano, tunaye mgobea kiti cha ugavana Margaret Wanjiru...tushinde au tushindwe hiyo ni demokrasia

lakini tusipindishe sheria ili tuweze kuepuka ushindani, tuko tayari."Murkomen aliongea.

Kwa ujasiri Wanjiru alikuwa na haya ya kusema,

 

"“Leo imekuwa siku njema sana, nimeweza kupata certificate yangu ya nomination pamoja na kuzindua chama chetu cha UDA ambayo itasaidia watu wengi kuinuka kisiasa. Tunamshukuru Mungu, tunajua kuna makesi kortini lakini tunatarajia Mungu atatupatia ushindi. Na nataka kuwaambia watu wa Nairobi musife moyo, hii ushindi ni wetu." Aliongea Margaret.

Ni wazi kwamba kinyang'aro cha uaniaji kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi kitakuwa cha kupambana na kikali.

View Comments