In Summary
  • Agnes Kavindu awasihi wakazi wa Mahakos wamchague
  • Ni uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Machi,18,2021.

Kampeni za useneta katika kauntii ya Machakos zinaendelea kupigwa kwa mpigo, huku wawaniaji tofauti wakizunguka nchini na kuwasihi wananchi wawapigie kura.

Mnamo Jumapili mwaniaji useneta kupitia tiketi ya Wiper, na aliyekuwa mkewe aliyekuwa seneta wa Machakos Muthama,Agnes Kavindu aliwasihi wakazi wa Mlolongo wampigie kura.

PIa aliendelea na kuwaeleza kwamba hana kazi wala chochite kwa hivyo wanapaswa kucchukua fursa hiyo na kumwajiri.

 

Ni uchaguzi ambao umepangwa kufanyika Machi,18,2021.

“Mimi ninawauliza nyinyi watu wa Machakos, mnapenda wamama? Si mnipatie kazi tu nijifanyie kazi, kwa maana mimi sasa sina bwana, sina lolote, sina kazi, si mniajiri kazi tu?” Alizungumza Kavindu.

Mwanasiasa huyo aliandamana na mbunge wa Matungulu Stephen Mule, mwakilishi wa akina mama wa kaunti ya Machakos Joyce Kamene,mwanasiasa Kalembe Ndile miongoni mwa wengine.

Wanasiasa hao pia walimpgia debe Kavindu na kusema kwamba anaweza kuwa seneta wa Machakos.

 

 

 

 

 

 

View Comments