In Summary
  • Spika wa bunge la Seneti Kenneth Lusaka ameamuru kuwasilishwa kwa Muswada wa Katiba ya Kenya (Marekebisho) ya mwaka 2020 uahirishwe
  • Haya yalijiri baada ya  agizo la spika Jumatano kwamba Muswada huo uletwe kwa njia ambayo IEBC iliwapeleka kwa bunge za Kaunti
Spika wa Seneti Ken Lusaka. Picha: HISANI

Spika wa bunge la Seneti Kenneth Lusaka ameamuru kuwasilishwa kwa Muswada wa Katiba ya Kenya (Marekebisho) ya mwaka 2020 uahirishwe.

Muswada huo ulikuwa umepangwa katika karatasi ya agizo ili kuletwa katika Bunge ili uweze kusomwa siku ya Alhamisi Machi 4.

Haya yalijiri baada ya  agizo la spika Jumatano kwamba Muswada huo uletwe kwa njia ambayo IEBC iliwapeleka kwa bunge za Kaunti.

Lakini mnamo Alhamisi, spika alisema kuwasilishwa  kwa Muswada huo kutaahirishwa hadi tarehe nyingine.

"Baada ya kushauriana na kamati yetu ya maswala ya sheria na ile ya Bunge, ningependa kutofautisha Agizo Namba 8. Nitatoa habari zaidi baadaye," Lusaka alisema.

View Comments