WHO Shirika la afya nchini

Mataifa hayapaswi kusitisha matumizi ya chanjo ya corona ya AstraZeneca kwa kuhofia kusababisha kuganda kwa damu wakati hakuna ukweli wowote juu ya hilo, Shirika la Afya Duniani limesema.

Bulgaria, Denmark na Norway ni miongoni mwa mataifa ambayo yamesitisha matumizi ya chanjo hiyo.

Lakini Ijumaa, msemaji wa WHO amesema hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.

Margaret Harris amesema chanjo hiyo ni salama na iendelee kutumika.

Watu wapatao milioni 5 barani ulaya tayari wamepata chanjo hiyo ya AstraZeneca.

Kuna kesi zipatazo 30 barani ulaya za watu kupata madhara ya kuganda damu baada ya kuchanjwa chanjo hiyo.

Kuna ripoti ya mwanamke mwenye umri wa miaka 50-aliyefariki baada ya kuganda damu alipopata chanjo hiyo.

WHO inafanyia uchunguzi taarifa hiyo, kama kuna maswali yeyote kuhusu usalama, Bi Harris alisema.

Lakini hakuna uhusiano wowote wa matatizo ya kiafya ulioripotiwa kutokana na chanjo hiyo, aliongeza.

Bulgaria imeamua kusitisha kutoa chanjo hiyo kama vile Denmark, Iceland na Norway pamoja na Thailand. Italia na Austria zimeacha kuendelea kutumia dozi hiyo pia kwa kuchukua tahadhari tu.

"Niliagiza kusitishwa kutolewa kwa chanjo ya AstraZeneca mpaka wakala wa dawa Ulaya atakapotuthibitishia mashaka yote yaliyopo juu ya usalama wa dozi hiyo," alisema waziri mkuu wa Bulgarian, Boyko Borisov .

Shirika la madawa la Muungano wa Ulaya(EMA) lilisema awali kwamba hakuna dalili kwamba chanjo hiyo inasababisha kugada kwa damu mwilini, likiongeza kuwa ni "faida ambayo zinaendelea kuwa kubwa kuliko hatari zake.

AstraZeneca ilisema kuwa usalama wa dawa umefanyiwa utafiti mkubwa katika majaribio ya tiba, ikiwa ni pamoja na katika maabara za Ureno, Australia, Mexico na Ufilipino ,wamesema kuwa wanaendelea na mpango wa utoaji wa chanjo.

Mataifa mengine ambayo yanataka kusitisha ni pamoja na Uingereza, Ujerumani ,Mexico na Australia.

View Comments