Kiongozi wa ODM Raila Odinga amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu kuambukizwa Covid-19.

Katika kanda iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii, Raila anaonekana akifanya mazoezi mepesi nje ya nyumba yake huku binti yake Winnie akimpa moyo.

"Ni jambo nzuri. Nafurahia sana kurudi nyumbani ... huko kulikuwa kama gereza. Ni vizuri kupumua hewa safi na angalau kuona maumbile," Raila aliyekuwa na furaha alisema.

Akiwa amevalia nguo za mazoezii, kofia na barakoa, kiongozi wa ODM hata hivyo alithibitisha kuwa bado amejitenga hadi apate nafuu.

Raila alikimbizwa hospitalini usiku wa Jumanne baada ya kuhisi uchovuĀ  na maumivu.

Siku ya Alhamisi jioni Raila alifichua kwa umma kuhusu hali yake ya kiafya na kutangaza hadharani kuwa alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.

View Comments