In Summary
  • Kiongozi wa Upinzani Tanzania Tundu Antiphas Lissu amesisitiza kuwa habari za kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, hazikumshangaza
Tindu Lissu
Image: Maktaba

Kiongozi wa Upinzani Tanzania Tundu Antiphas Lissu amesisitiza kuwa habari za kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, hazikumshangaza.

Akiongea Alhamisi, Lissu alisema alitarajia habari hizo, tangu mara ya kwanza alipoandika kwenye ukurasa wake wa  twitter akihoji Rais Magufuli yuko wapi, kwani alikuwa amepokea habari za kuaminika kuwa anaumwa sana.

"Nimepata habari za kupita kwa Magufuli bila mshangao wowote. Nilitarajia hii yote tangu siku ya kwanza nilipotumia barua pepe mnamo Machi 7

 

Nilipouliza swali Rais Magufuli yuko wapi na hali yake ya kiafya ni nini kwa sababu wakati huo nilikuwa na habari kutoka kwa vyanzo vya kuaminika kutoka kwa serikali kwamba rais alikuwa mgonjwa sana na covid-19 na hali yake ilikuwa mbaya sana.

Habari kwangu haikushangaza hata kidogo, kitu pekee kinachonishangaza ni ukweli kwamba wanaendelea kusema uwongo hata sasa kwa kuwa amekufa," Alisema Lissu.

Tindu alitaka kujua kwanini afya yake Magufuli ilifichwa wananchi licha yake kuwa kiongozi wa taifa.

"Afya ya Rais ni suala la umma. Kikwete alipotibiwa tezi dume Marekani tuliambiwa. Mkapa alipotibiwa nyonga Uswisi tulijulishwa. Baba wa Taifa alipougua saratani ya damu London hatukufichwa. Kwa nini kuna kigugumizi juu ya afya ya Rais Magufuli? Au ndio kila zama na kitabu chake?" iuliza Tindu Lissu.

 

 

 

View Comments