21 March 2021 1 Min Read
DCI yamkamata mwalimu kwa tuhuma za kumshambulia mwanafunzi
In Summary
- Wapelelezi pia waamsaka mwalimu wa pili aliyejulikana kama Mike Kioko ambaye alikwepa wavu wa polisi
by Grace Muia Habari
Wapelelezi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamemkamata Joseph Nduva mwalimu wa shule ya step up zion makueni kwa madai ya kumlawiti mwanafunzi wakati wa safari ya shule.
Wapelelezi pia waamsaka mwalimu wa pili aliyejulikana kama Mike Kioko ambaye alikwepa wavu wa polisi.
Kulingana na ripoti ya polisi walimu hao wawili wa Step Up Zion walionekana na shahidi akiwapiga wasichana wawili wa shule kwenye bwawa la kuogelea Jumamosi.
Shahidi huyo aliwaita polisi, lakini mmoja wa washukiwa alifanikiwa kutoroka wakati wa kukamatwa .
Bwana. Nduva atafikishwa kortini siku ya Jumatatu wakati uchunguziunaendelea na kusakwa kwa mshukiwa huyo mwingine kukiendelea.